Madereva wa Serikali wanaokiuka sheria waadhibiwe

0
255

Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Madereva wa Serikali amewataka waajiri wote kuchukua hatua stahiki kwa madereva wote wa Serikali wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma.

Bashungwa anawaelekeza waajiri kuwasimamia ipasavyo madereva wote na kufanya nao vikao vya mara kwa mara ili kujua changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi na kuwakumbusha namna bora ya utunzaji wa vyombo hivyo vya moto walivyokabidhiwa.

Waziri Bashungwa amesema hayo akieleza masikitiko yake juu ya video fupi inayomwonesha dereva wa Serikali aliyesababisha ajali kwa kuendesha gari akiwa amelewa.

Aidha, ameeleza kusikitishwa na tabia ya baadhi ya madereva kuendesha magari bila kuzingatia Sheria za Barabarani na kuegesha magari katika maeneo yasiyo salama na hivyo kusababisha ajali, uharibifu wa magari au kuhatarisha maisha na mali za Wananchi.