Madai yote yalipwe ndani ya siku 60

0
222

Rais Samia Suluhu Hassan amamuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhakikisha anasimamia madai ya Bima ya Afya na tatizo la waajiri kutowasilisha michango ya wafanyakazi.

Akizungumza kuhusu Bima ya Afya Rais Samia amemuagiza Waziri Mkuu Majaliwa kusimamia madai ya watoa huduma yanayopaswa kulipwa ndani ya siku 60 tangu kupokelewa kama inavyosema sheria ya bima ya afya sura ya 395.

“Kama mtu alijilimbikizia, ndani ya siku 60 alipe malimbikizo yote, wafanyakazi wafaidike na bima zao za afya,” amesema Rais Samia.

Kufuatia tatizo la waajiri kutowasilisha michango ya Wafanyakazi, Waziri Mkuu ataitisha kikao na waajiri ili kuondoa tatizo la hilo.