Mabalozi 23 walioteuliwa na Rais leo

0
463

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mabalozi 23 kama ifuatavyo;

  1. Amemteua Lut. Jen. Yakub Hassan Mohamed. Lut. Jen. Yakub ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
  2. Amemteua Mej. Jen. Richard Mutayoba Makanzo. Mej. Jen. Makanzo ni Mkuu wa Kamandi ya Wanamaji ya JWTZ.
  3. Amemteua Pereira Silima. Silima ni Naibu Waziri Mstaafu wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
  4. Amemteua Maulidah Bwanaheri Hassan. Maulidah ni Msaidizi wa Rais Diplomasia, Ofisi ya Rais Ikulu.
  5. Amemteua Togolani Edriss Mavura. Bw. Mavura ni Msaidizi wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete.
  6. Amemteua Edwin Rutegaruka. Rutegaruka ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).
  7. Amemteua Fredrick Kibuta. Kibuta ni Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais, Ikulu.
  8. Amemteua Noel Emmanuel Kaganda. Kaganda ni Afisa Medani, Ofisi ya Rais, Ikulu.
  9. Amemteua Mindi Kasiga. Mindi ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
  10. Amemteua Caroline Kitana Chipeta. Chipeta ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  11. Amemteua Macocha Tembele. Tembele ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  12. Amemteua Agnes Kayola. Kayola ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  13. Amemteua Masoud Abdallah Balozi. Balozi ni Kaimu Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje – Zanzibar, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  14. Amemteua Ceasar George Waitara. Waitara ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  15. Amemteua Swahiba Habib Mndeme. Mndeme ni Afisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania Washington D.C nchini Marekani.
  16. Amemteua Said Juma Mshana. Mshana ni Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais, Ikulu.
  17. Amemteua Alex Gabriel Kallua. Kallua ni Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais, Ikulu
  18. Amemteua Mahmoud Thabit Kombo. Kombo ni Waziri Mstaafu wa Utalii na Mambo ya Kale, Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, Zanzibar.
  19. Amemteua James Gillawa Bwana. Bw. Bwana ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Shinyanga.
  20. Amemteua Hoyce Temu. Temu ni Mwandishi wa Habari na Mjasiriamali.
  21. Amemteua Said Shaib Mussa. Said ni Naibu Mkurugenzi, Ofisi ya Rais, Zanzibar.
  22. Amemteua Elsie Sia Kanza. Kanza ni Mshauri Maalum wa Rais kwenye Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum).
  23. Amemteua Robert Kainula Kahendaguza. Kahendaguza ni Naibu Balozi, Umoja wa Mataifa, Geneva.

Uteuzi wa Mabalozi hawa umeanza leo Mei 22 2021 na wataapishwa kwa tarehe zitakazotangazwa baadaye.