Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la mawaziri.
Kwanza, Rais amemteua Angellah Kairuki kuwa Mbunge na kisha kumteua kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI).
Aidha, Rais Samia amemteua Dkt. Stergomena Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Awali Dkt. Stergomena alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa.
Rais pia amemteua Innocent Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa akichukua afasi ya Dkt. Stergomena.
Kabla ya uteuzi huo Bashungwa alikua waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI).
Viongozi wote wataapishwa Oktoba 3, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam.