Maandalizi ya uzinduzi wa Royal Tour yapamba moto

0
1185

Watu elfu tano kutoka maeneo mbalimbali nchini wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi wa filamu ya Royal Tour jijini Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongella amesema kuwa uzinduzi huo utafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Amesema mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo pia Viongozi wengine wa ngazi ya juu wanatarajiwa kuhudhuria.

Mongella amesema hali ya ulinzi na usalama imeimarishwa mkoani humo, hivyo wageni wote watakaofika mkoani humo kwa ajili ya uzinduzi huo wasiwe na wasiwasi.

Filamu ya Royal Tour inazinduliwa kwa mara ya kwanza jijini Arusha baada ya kuzinduliwa rasmi nchini Marekani.

Baada ya kuzinduliwa jijini Arusha, uzinduzi mwingine wa filamu hiyo utafanyika Zanzibarb pamoja na Dar es Salaam.