Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amesema, maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru yamekamilika.
Profess Ndalichako amezungumza hayo katika uwanja wa CCM Sabasaba mkoani Njombe ambapo mbio za Mwenge wa Uhuru zitanduliwa Aprili 2, 2022 na mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.
“Niseme tu maandalizi yamekamilika na kesho ndio tukio lenyewe litafanyika hapa [uwanja wa Sabasaba] kwa hiyo niwaalike Wananchi kutoka sehemu mbalimbali wafike wshiriki shughuli hii.”amesema Profesa Ndalichako
Ameongeza kuwa Mwenge wa Uhuru utapita katika halmashauri za mikoa yote nchini.
“Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kwa siku 195 katika halmashauri na mikoa yote 31 nchini na zoezi litahitimishwa tarehe 14 Oktoba 2022, mgeni rasmi atakuwa Rais Samia Suluhu Hassan.”ameongeza Profesa Ndalichako