Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa maagizo matano kwa Wizara ya Madini na sekta zinazohusika ili kuhakikisha zinaboresha sekta ya madini nchini.
Maagizo hayo ni;
- Kusimamia utekelezaji wa maadhimio yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa Kimaataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania mwaka 2022, ili taarifa za utekelezaji ziwasilishwe kwenye mkutano ujao.
- Wizara ya Madini kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vidhibiti utoroshaji wa madini, na kuhakikisha biashara hiyo inafanyika kisheria.
- Wizara iimerishe ushirikishwaji wa wadau kwenye masuala mbalimbali kwa kuimarisha mawasiliano na wadau wa madini, ili kuwa na mfumo sahihi wa kuwasilisha na kutatua changamoto zinaazowakabili.
- Wizara kwa kushirikiana na TAMISEMI zibainishe na kutambua maeneo ya masoko na viwanda vya madini.
- Wizara hiyo iendelee kuvinadi viwanda vya ndani kwa kazi vinavyofanya ikiwemo kusafisha madini, ili kuvutia wateja kutoka ndani na nje ya nchi.