Lowassa kuagwa Dar Februari 13

0
255

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa aliyefariki dunia Februari 10, 2024 ataagwa Februari 13, 2024 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Majaliwa amesema hayo nyumbani kwa marehemu Lowassa jijini Dar es Salaam wakati akitoa ratiba ya mazishi ya Kiongozi huyo.

Amesema Ibada ya kumuaga Lowassa itafanyika Februari 14, 2024 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front mkoani Dar es Salaam.

Mwili wa Lowassa utasafirishwa Februari 15, 2024 kwenda nyumbani kwao Monduli mkoani Arusha na kuagwa Februari 16, 2024

Atazikwa Februari 17, 2024 ambapo mazishi hayo yataongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.