Lori aina ya Scania lenye namba za usajili T850 DUH lililobeba mchele kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani Arusha limepinduka eneo la Kimange mkoani Pwani na kukata mawasiliano ya Barabara ya Msata – Segera.
Ajali hiyo imetokea saa tisa alasiri leo na kupelekea shughuli za usafiri kukwama wa zaidi ya saa nne, kabla ya lori hilo kuondolewa na kuruhusu magari kuendelea na safari.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge naye alifika katika eneo la tukio na kujionea hali halisi na kutoa maelekezo kwa Askari wa usalama barabarani kushirikiana na wananchi ili kusaidi kulinasua lori hilo ili wananchi waendelee na safari.
Hakuna mtu yeyote aliyeumia kutokana na ajali hiyo.