Lissu afutiwa kesi ya uchochezi

0
237

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopo mkoani Dar es Salaam, imeifuta kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleao (CHADEMA) kwa upande wa Bara Tundu Lissu na wenzake watatu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuieleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Katika kesi ya msingi, Lissu na wenzake walishtakiwa kwa kosa la kula njama na mhariri wa gazeti la Mawio ili kutoa machapisho kwenye gazeti yenye maneno ya uchochezi.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Simon Mkina, Jabir Idrisa na mchapishaji wa kampuni ya Jamana Ismail Mehbooh.