Kufuati tishio la Kimbunga Kenneth katika mikoa ya Mtwara na Lindi, mkoa wa Lindi umetangaza kuahirishwa kwa maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani yaliyokua yafanyike mkoani humo.
Akitangaza Uamuzi huo, Mkuu wa mkoa wa Lindi, – Godfrey Zambi amesitisha pia shughuli zote za serikali na kuwataka wakazi wa mkoa huo kuacha kupuuza tahadhari inayoendelea kutolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) kuhusu kimbunga Kenneth.