Lindeni miradi ya TASAF iwanufaishe

0
287

Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia, Edna Kashangaki ameshauri kuwepo na usimamizi madhubuti wa miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) hasa ile ya upandaji miti, ili idumu na kuendelea kuwa na manufaa kwa wananchi.

Kashangaki ametoa ushauri huo baada ya timu ya wawakilishi kutoka Benki ya Dunia kutembelea vijiji vya Gidangu na Mulba wilayani Hanang’ mkoani Manyara, kujuonea miradi mbalimbali inayokelezwa na TASAF katika kuziinua kimaisha kaya maskini.

Wawakilishi hao kutoka Benki ya Dunia wapo mkoani Manyara kufuatilia utekelezaji wa miradi ya kuziinua kaya maskini ambapo wamefurahishwa na miradi hiyo kwani licha ya kupatiwa fedha kidogo wamefanya mambo makubwa.