Lema apelekwa Singida kwa mahojiano

0
358

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike amethibitisha kukamatwa kwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kuhusu mauaji ya watu 14 wilayani Manyoni kati ya mwaka 2019 na mwaka huu.

Kamanda Njewike amewaambia waandishi wa habari mkoani Singida kuwa, Lema amekamatwa mkoani Arusha na kusafirishwa hadi mjini Singida kwa ajili ya kufanyiwa mahoajiano kuhusu suala hilo.