Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza kupanda kwa bei za nauli za mabasi ya kwenda mikoani na huduma ya Usafiri wa Mabasi ya Mijini Maarufu (DALADALA).
Akitangaza Nauli hizo jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Gillard Ngewe amesema bei hizo zimepanda kufuatia Maombi ya watoa huduma ya Usafiri Nchini.
Ngewe amesema baada ya kufanya ukokotoaji kwa mujibu wa sheria ya LATRA ya mwaka 2019 na kanuni ya Tozo ya mwaka 2020 Mamlaka imetangaza viwango vyopya kama ambavyo wadau walipendekeza.
Amesema viwango hivyo vipya vinahusisha mabasi yanayotoa huduma ya usafiri kwenye mikoani nan chi za jirani amabzo zimepanda kwa asilimia 11.92 kwa Daraja la kawaida na asilimia 6.88 kwa daraja la kati
Ngewe amesema, bei hizo pia zimehusisha mabasi yanayotoa huduma maeneo ya mijini (Daladala) ambapo nauli imepanda kutoka shilingi mia nne (400) hadi mia tano (500) kwa umbali mfupi wa Kilomita 0 hadi 10 na umbali mrefu wa Kilomita 36 hadi 40 kwa Sh.1100.