Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. John Magufuli akiwa ameambatana na Mgombea Mwenza, Makamu wa Rais, Samia Suluhu leo wamefika katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambapo wamechukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kwa muhula wa pili.
Baada ya zoezi hilo, viongozi hao wamefika katika ofisi za Makao Makuu ya CCM, Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengi wamezungumza mamia ya wananchi waliojitokeza, pamoja kuanza kutafuta wadhamini.
Hapa chini ni picha zinazoonesha matukio mbalimbali ya kuchukua fomu na kuzungumza na wananchi: