Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Aisha Dachi na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawssiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba, wakisaini hati za makabidhiano za mradi wa usikivu wa kurushia matangazo ya TBC Taifa na Bongo FM wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) leo Aprili 15, 2024.
Mradi huo umezinduliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko ambapo amezindua mradi wa Loliondo – Ngorongoro kwa niaba ya vituo vingine ambavyo ni Makete, Kyela, Uvinza na Mbinga kwenye kiwanja cha Kassim Majaliwa Majaliwa.