Kunenge ambana mkandarasi Barabara ya Makongo

0
356

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge amemuagiza mkandarasi anayejenga Barabara ya Makongo kuhakikisha inakamilika kabla ya Oktoba 2021.

Kunenge ametoa agizo hilo mapema leo alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo ambayo inatarajiwa kupunguza foleni kwa wakazi wa mkoa huo, mathalani katika Barabara ya Bagamoyo.

Aidha, amezitaka DAWASA na TANESCO kufanya kazi kwa ushirikiano na mkandarasi huyo kwa kuondoa miundombinu ya maji na umeme iliyopita kwenye mradi ili mkandarasi asipate kisingizio chochote cha kuchelewesha kazi.

Ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 4.5 unagharimu TZS bilooni 8.2.