Kopo la maji lasababisha vifo

0
240

Watoto wawili Jeplus Marco (3) na Martin Lameck (1) wamefariki baada ya kuzama kisimani wakiwa wanafuata kopo lililokuwa linaelea kisimani katika Mtaa wa Nyantorotoro B, Halmashauri ya Mji Geita.

Mwakilishi wa Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, Emmanuel Ndosi amethibitisha kutokea tukio hilo jana jioni, huku akitoa rai kwa wananchi kuwalinda watoto hasa wanaoishi katika maeneo karibu na visima vya maji na mabwawa ili kuepuka matukio ya watoto kupoteza maisha.

Afisa Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Nyantorotoro, Khadija Mzee ameagiza kufunikwa visima, madimbwi pamoja na mashimo yote.

Wazazi wa watoto hao wamesema waliwaacha watoto nyumbani wakicheza wakati wakiwa wameenda shambani kulima.