Kongamano la mahakama za kikanda lazinduliwa

0
139

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la   Mapinduzi  Dkt. Hussein Mwinyi  amesema uamuzi wa kufanyika  kwa kongamano la mahakama za kikanda na kitaifa barani Afrika, kutainufaisha Zanzibar na kuwawezesha Majaji na Viongozi mbalimbali wa kada ya sheria kushiriki na kuwaongezea maarifa na uzoefu.

Dkt. Mwinyi amesema hayo katika uzinduzi wa kongamano la mahakama za kikanda na kitaifa Barani Afrika lililofanyika Zanzibar.

Amesema kongamano hilo ni muhimu kwa maendeleo na  ufanisi wa mahakama pamoja  na kada ya sheria nchini, jambo  litakalowawezesha  washiriki wakiwemo  majaji na wataalam wengine wa kada hiyo kupata maarifa na uzoefu.

Kwa mujibu wa Dkt.Mwinyi, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimeweka kipaumbele katika utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu kama zilivyobainishwa katika katiba zao.

Ameyataja mambo kadhaa  yanayolalamikiwa  na kudhihirisha uvunjaji wa haki za binadamu kwa jamii, kuwa ni pamoja na baadhi ya makundi kunyimwa haki za msingi, uonevu, ukatili, unyanyasaji na kutokuwepo uhuru katika masuala muhimu pamoja na ubaguzi wa aina mbalimbali.

“Tumeunda Tume ya Haki za Baindamu katika Utawala Bora inayoendelea kufanya kazi vizuri katika kuimarisha Haki za Bainadamu katika pande zote mbili za Muungano wetu”, amesema Dkt. Mwinyi
.