Viongozi wa dini mbalimbali nchini wanatarajia kuwa na kongomano la kuliombea taifa na kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi bora tangu aingie madarakani.
Wakizungumza na waandishi wa habari Jijini Mbeya viongozi hao kutoka mikoa tofauti tofauti wamesema wameamua kuandaa kongamano hilo kutokana na kutambua juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuleta maendeleo kwa taifa na wananchi kwa ujumla
Viongozi wa dini kutoka madhehebu tofauti nchini ambao wamekusanyika jijini mbeya kuelekea kwenye kongamano la kitaifa la kuliombea taifa na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa utendaji uliotukuka.
Mwenyekiti wa kongamano hilo Profesa Donard Mwanjoka anasema kongamano hilo linatarajiwa kuwa na watu zaidi ya mia nane na litafanyika katika ukumbi wa tughimbe jijini Mbeya.