Kocha wa makipa Simba matatani kwa dawa za kulevya

0
139

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA)
imewakamata watu tisa kwa tuhuma za kukutwa na kilo 34.89 za dawa za kulevya aina ya Heroin.

Kamishna Jenerali wa DCEA Gerald Kusaya amewaambia waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam kuwa, watu hao tisa ni pamoja na mmiliki wa Kambiaso Sports Academy Alhaji Kambi Zubeir Seif na kocha wa makipa wa klabu ya Simba, Mwalami Sultan.