Kizimbani kwa tuhuma za kusafirisha bangi

0
229

Mtu mmoja amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shitaka moja la kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi kilogramu 446.11

Mshitakiwa huyo Frank Mwita amefikishwa mahakamani hapo na kusomewa shitaka lake na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Agustina Mpando.

Wakili Wankyo amedai mshitakiwa huyo alikamatwa na dawa hizo Februari 25 mwaka huu Kurasini mkoani Dar es Salaam.

Hata hivyo wakili Wankyo amedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika hivyo kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine kutajwa.

Hakimu Mbando ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 3, 2021 itakapotajwa.