Kituo kipya cha mabasi chaizima Ubungo

0
332

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amezindua rasmi Stendi Kuu ya Magufuli jijini Dar es Salaam (Magufuli Bus Terminal), Mbezi Luis leo Februari 24, 2021.

Kituo hicho ambacho ni cha kimataifa ndicho kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge amesema matumizi ya kituo hicho yatapunguza adha ya usafiri jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi wa kituo kikuu cha mabasi chenye uwezo wa kuhudumia zaidi ya abiria laki mbili (200000) kwa siku ndiyo mwisho wa matumizi ya kituo kilichozoeleka cha Ubungo.

Kuanzia kesho Februari 25, mabasi yote ya mkoani yataanza safari zake katika kituo cha Magufuli.