Akijibu swali la Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma, Peter Mavunde na mchangiaji mada mwingine kuhusu kitabu cha “Continuity with Vision: The Roadmap to Succes for President Samia Suluhu Hassan”
kupatikana kwa lugha ya Kiingereza, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha amesema kitabu hicho kimeandikwa kwa lugha ya kimataifa ili kuwafikia watu wengi zaidi duniani.
Akizungumza jijini Dodoma wakati wa Kongamano la kukichambua kitabu hicho Dkt. Rioba amesema,
huu ni mwanzo na kwamba Wanazuoni walioandika kitabu hicho wako mbioni kuandika muhtasari wake kwa lugha ya Kiswahili na baadaye kitabu kamili kitafuata.
Zaidi ya Wanazuoni 40 wameshiriki kuandika kitabu hicho cha “Continuity with Vision: The Roadmap to Succes for President Samia Suluhu Hassan” (Muendelezo wa Maono katika Safari ya Mafanikio ya Rais Samia Suluhu Hassan chenye jumla ya sura 29.