Kiswahili sasa rasmi Afrika Kusini

0
227

Tanzania na Afrika Kusini zimesaini makubaliano ya Kiswahili kufundishwa katika shule za msingi za nchini humo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda na Waziri wa Elimu wa Afrika Kusini, Angelina Motshekga wamesaini hati za makubaliano hayo mbele ya Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango katika maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yanayofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Hizi ni jitihada za kukuza lugha ya Kiswahili na kuendelea kutambuliwa zaidi Duniani.