Kindamba : Simamieni ukarabati hospitali ya Pangani

0
168

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amewataka watendaji waliopewa dhamana ya kusimamia ukarabati wa hospitali ya wilaya ya Pangani kufanya kazi kwa weledi ili kwenda sawa na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali ambayo ni shilingi Milioni 900.

Kindamba ametoa wito huo alipokua akizungumza na viongozi wa hospitali hiyo pamoja na Wajumbe wa kamati ya uongozi na fedha wa halmashauri ya wilaya ya Pangani, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi wilayani humo.

Amesema ni vema kila moja akasimama kwenye nafasi yake katika kutimiza wajibu wake ili kufikia malengo yaliowekwa na Serikali ambayo ni kuwasogezea karibu Wananchi huduma bora za afya.