Mkuu wa mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo kushirikiana na watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kudhibiti bidhaa za magendo zinazoingia nchini kinyume na utaratibu.
Kindamba ametoa kauli hiyo jijini Tanga wakati akizindua boti maalum yenye thamani ya shilingi Bilioni 529.
Amesema kila mmoja anapaswa kuwa makini, kwani bidhaa zilizoingia nchini kinyume na utaratibu kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 pekee ni za shilingi Bilioni 11 na Milioni 54, huku kodi yake ikiwa ni zaidi ya shilingi Bilioni 13.
Kati ya fedha hizo kodi iliyokwepwa kwa mkoa wa Tanga pekee ni shilingi Milioni 796.