Kindamba apokelewa Tanga

0
175

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amewataka watumishi wa mkoa huo kufanya kazi kwa umoja na mshikamano, huku wakitanguliza mbele maslahi ya Taifa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Kindamba ametoa kauli hiyo mara baada ya kupokelewa na watumishi wa mkoa huo pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali.

Ametokea mkoani Songwe ambako alikua akihudumu kwa nafasi hiyo ya Mkuu wa mkoa kabla ya kuhamishiwa mkoani Tanga hivi karibuni.