Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imemkamata mfanyabiashara anayedaiwa kuwa ni Kinara wa mtandao wa biashara ya dawa za kulevya aina ya Cocaine pamoja na kukamata gramu 692.336 za dawa hizo.
Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas Lyimo
amesema mfanyabiashara huyo alikuwa akitafutwa tangu mwaka 2000 na amekamatwa katika eneo.la Boko, Dar es Salaam akiwa pamoja na washirika wake watatu.
Kamishna Jenerali Lyimo amesema mfanyabiashara huyo ana mtandao mkubwa wa wasafirishaji ambao huwatumia kusafirisha dawa za kulevya kwenda mataifa mbalimbali.
Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini
Imewataka Wananchi kutojihusisha na biashara ya dawa za kulevya kwani inaendelea na oparesheni nchi kavu na majini.