KINANA APONGEZA KUUNDWA WIZARA YA MIPANGO

0
156

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Abdulrahman Kinana amepongeza uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan Hassan wa kuunda wizara inayohusika na mipango.

Pia, amepongeza hatua ya kuifanya Tume ya Mipango kuwa chini ya Ofisi ya Rais ambapo amesema itaongeza kasi na uhakika wa mipango ya maendeleo nchini.

Kinana ameyasema hayo wilayani Kibiti mkoani Pwani kupitia mkutano wa hadhara uliondaliwa na Mbunge wa jimbo la Kibiti, Ally Mpembenwe kwa lengo la kueleza kazi ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM iliyofanyika katika jimbo hilo.

“Hivi karibuni Rais ameunda wizara mpya inayoshughulika na mipango, kwa lugha nyingine ni Tume ya Mipango ambayo ipo ofisini kwake, lengo lake moja tu, tumekuwa tukifanya mambo mengi nchi hii lakini bila mipango mizuri, Rais akaona wizara ile inapoitwa Wizara ya Fedha na Mipango inafanya kazi zaidi ya kukusanya na kutumia kuliko kupanga akaona hapana, nadhani ni vizuri sasa tutengeneze wizara ya mipango,” amesema Kinana.