Kinana afanya ziara Katavi

0
233

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Abdulrahman Kinana amewasili mkoani Katavi kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Kinana aliyeongozana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Taifa, Shaka Hamdu Shaka, amewataka Wanawake na Vijana nchini kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama, ambacho kinafanya uchaguzi wake mkuu mwaka huu.

Mapema Kinana akiwa pamoja na mwenezi Taifa, amezindua maduka zaidi ya 200, mradi wa CCM mkoa wa Katavi pamoja na kituo cha afya Itenka kilichopo katika halmashauri ya wilaya Nsimbo kinachotarajiwa kuwahudumia wananchi zaidi ya elfu hamsini.