Kimbunga Ida chaleta madhara

0
137

Kimbunga Ida kinaendelea kuleta madhara makubwa katika maeneo mbalimbali nchini Marekani, ikiwa ni pamoja na kuharibu majengo kadhaa na miundombinu ya nishati ya umeme kwenye jimbo la Louisiana.

Watabiri wa hali ya hewa nchini Marekani wamesema, kimbunga Ida kina upepo unaosafiri kwa kasi ya zaidi ya kilometa 240 kwa saa.

Kufuatia kimbunga hicho, Rais Joe Biden ameahidi kuwa Serikali yake itandelea kutoa msaada kwa watu wote walioathiriwa na kimbunga hicho kadri itakavyohitajika.

Amewataka watu wanaoishi kwenye maeneo ya pwani kuondoka na kutafuta hifadhi kwenye maeneo salama, kwani kimbunga hicho kinasababisha mafuriko makubwa.