“Ndugu zangu huwa mmanisikia ninapoapisha watendaji baada ya kuwateua nawaambia nenda kama kuna mtu unaona anakurudisha nyuma niletee aondoke, kama ni level ya chini sio yangu ondoeni fanyeni mabadiliko mnayoona mtakwenda vizuri.
Sasa wale wanaobadilishwa ni zogo ni kelele na kila mtu ana Godfather wake, hao Ma Godfather tena mbio kwa Rais.
Kama unabadilishwa hutaki kubadilishwa onesha unaweza, unafanya kazi unaonesha ufanisi hutaondoshwa. Lakini kama unazubaisha unababaisha huwezi utaondoka. Kwa hiyo niwaambie wakuu wa mashirika msiogope kufanya mabadiliko kelele zipo hazitaondoka, msiogope kufanya mabadiliko wekeni watu ambao watakwenda na ile kasi tunayoitaka.”
Rais Samia Suluhu Hassan