Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya Wadau wa Demokrasia ya vyama vingi vya siasa kimependekeza Tan’zania ianze harakati ‘za kupata katiba mpya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Akisoma mapendekezo ya awali ya kikosi kazi hicho Ikulu mkoani Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kikosi kazi hicho Profesa Rwekaza Mukandala amesema muda huo ni muafaka kwa kuwa hautaathiri uchaguzi mkuu ujao.
Kikosi kazi hicho cha kuratibu maoni ya Wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa kina wajumbe 25 ambao wanaripoti moja kwa moja kwa Rais.
Kikosi hicho kiliundwa kwa lengo la kutoa mapendekezo ambayo yatawezesha masuala ya siasa kuendeshwa kwa tija.
Pia kikosi hicho kimependekeza kufanyiwa maboresho kwenye sheria na kanuni za uchaguzi ili kuondoa migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza wakati wa chaguzi mbalimbali.
Pendekezo jingine ni kuangaliwa upya kwa vigezo vya utoaji ruzuku kwa vyama vya siasa ambavyo vina usajili wa kudumu.