Jeshi la polisi mkoani Mtwara linamshikilia Hamis Athumani mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa kijiji cha Chingungwe wilaya ya Tandahimba, kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Mtwara Nicodemus Katembo amesema, Hamis anatuhumiwa kumuua baba yake Hamis Chipota mwenye umri wa miaka 50 baada ya baba yake kuingilia ugomvi wa familia uliokuwepo kati yake na mke wake.
Kaimu Kamanda Katembo amesema Hamis anadaiwa kufanya mauaji hayo tarehe 24 mwezi huu majira ya saa 12 jioni katika Kijiji cha Chingungwe.