Kihongosi Katibu Mkuu UVCCM

0
191

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana jijini Dodoma leo, imemchagua Kenan Kihongosi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

Kihongosi amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Arusha, na katika uteuzi wa hivi karibuni wa wakuu wa wilaya uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida.