Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amezishauri taasisi za umma ziwafuate na zijifunze mazingira na changamoto za Wafanyabiashara pamoja na kuwapa elimu kuhusu kodi, ada na tozo mbalimbali na sio kuwasubiri ofisini.
Kigahe ametoa ushauri huo mkoani Songwe wakati wa ziara yake mkoani humo ambapo ametembelea kiwanda cha Kahawa cha GDM na kiwanda cha Ilasi Sembe vilivyopo wilayani Mbozi pamoja na kuzungumza na Wafanyabishara wa mkoa huo.
Amewataka Wafanyabishara wa mkoa wa Songwe kuwa waadilifu, waaminifu, wawazi na wasioruhusu mianya ya rushwa katika ufanyaji biashara, ili kurahisisha jitihada za kupunguza tozo, faini, kodi na upatikanaji wa mikopo kwa riba nafuu hali ambayo itasaidia kukuza biashara zao, kuongeza ajira na kuongeza pato la Taifa kwa ujumla.