Kibaha haikukidhi vigezo kuwa Manispaa

0
137

Serikali imesema ilipokea wasilisho kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na kuchambua kwa kuzingatia vigezo vya kuupatia Mji wa Kibaha uliopo mkoani Pwani hadhi ya Manispaa ambapohaikukidhi vigezo. 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la  Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka aliyetaka kujua ni lini Serikali itaupatia Mji wa Kibaha hadhi ya Manispaa.

Serikali imesema ombi hilo kwa sasa lipo katika hatua za mwisho za uhakiki wa vigezo na mrejesho utatolewa kabla ya mwezi Juni mwaka huu.