Khalfan aanza kupatiwa matibabu

0
474

Siku moja baada ya TBC Digital kuonesha picha ya video ikimuonesha mtoto Khalfan Gideon wa mkoani Kigoma akiomba msaada wa matibabu kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Rais kutoa maelekezo kwa Wasaidizi wake kumtafuta mtoto huyo, leo Januari 28, 2024 Khalfan amefikishwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kigoma – Maweni na kuanza kupatiwa matibabu.

Mganga Mfawidhi wa hopsitali ya Rufaa ya Maweni Dkt. Stanley Binagi amesema uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha ugonjwa wa Khalfan kimeanzia katika genetics tangu akiwa tumboni.

Amesema kwa sasa wamenza kumpatia tiba za awali mtoto huyo wakati wanafanya utaratibu wa kuchukua sampuli za ngozi kwa ajili kuotesha ili kujua undani wa tatizo na hatimaye kumpatia tiba stahiki.

Mapema hii leo, mkuu wa mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amefika hospitalini hapo kumjulia hali mgonjwa huyo na kuwaagiza madaktari kuchukua hatua za haraka katika matibabu yake ili aweze kurudi shule kuendelea na masomo.