Mahakama wa Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha hadi mwezi Agosti mwaka huu
kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi Tisa wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo – CHADEMA akiwemo mwenyekiti wake Freeman Mbowe kutokana na ushahidi
upande wa jamhuri kutokamilika.
Akitoa tamko hilo Jijini Dsm Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Thomas Simba amesema
kesi hiyo imechukua muda mrefu na hivyo kuamua kusikilizwa kuanzia Agosti 5, 6
na 7 mfululizo mwaka huu ili hukumu kupatikana.
Mawakili upande wa serikali waliongozwa na Wakili Faraja Nchimbi kutokamilika
kutokana na kukosa vifaa vya kusapoti video ya Koplo Charles kama waya chaja na
projector ya kuonesha video hiyo.
Mnamo Februari 16 mwaka 2018, katika barabara ya Kawawa Kinondoni-Mkwajuni Mbowe
na wenzake 12 ambao hawakuwepo mahakamani wanadaiwa walikiuka tamko la kuwataka
kutawanyika ambako kugoma huko kulisababisha hofu na hatimaye kifo cha Akwilina
Akwiline na majeruhi kwa askari wawili.