Mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa Bukoba mkoani Kagera imeamuru kesi ya mauaji ya mwanafunzi wa shule ya msingi Kibeta,- Spelius Eradius inayowakabili walimu wawili wa shule hiyo kuhamishiwa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba ili kuanza kusikilizwa.
Uamuzi huo umetolewa na hakimu mkazi Mfawidhi John Kapokolo kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kisheria kusilikiliza kesi inayowakabili watuhumiwa hao.
Washitakiwa katika kesi hiyo ni mwalimu anayedaiwa kutoa adhabu ya kipigo kilichosababisha kifo cha Mwanafunzi ambaye ni Respicius Mutazangira pamoja na mwalimu mwingine anayedaiwa kupotelewa na mkoba uliodaiwa kupokelewa na marehemu,-Herieth Gerald.
Washtakiwa hao wamerudishwa rumande hadi hapo Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba itakapopanga tarehe ya kusikiliza shauri hilo.