Mahakama ya hakimu mkazi Mtwara kwa mara nyingine imeahirisha kesi ya mauaji inayowakabili maafisa saba wa Jeshi la Polisi nchini hadi tarehe 19 mwezi huu.
Akiahirisha kesi hiyo Hakimu Mkazi Mussa Essanju amesema upelelezi wa shauri hilo la mauaji namba 1/2022 bado haujakamilika.
Maafisa wa polisi wanaokabiliwa na kesi hiyo ya mauaji ni afisa upelelezi wa wilaya ya Mtwara, Gilbert Kalanje, mkuu wa kituo cha polisi Mtwara, Charles Onyango, afisa wa Intelijensia ya jinai mkoa wa Mtwara, Charles Kisinza, Mkaguzi wa Polisi, John Msuya pamoja na Mganga Mkuu wa zahanati ya polisi, Marco Mbuta.
Wengine ni Mkaguzi wa polisi, Shirazi Mkupa na Koplo Salum Mbalu.
Maafisa hao wanatuhumiwa kumuua Musa Hamis (25) ambaye ni mfanyabiashara wa madini na mkazi wa kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea mkoani Lindi, katika tukio lililotokea Januari 05 mwaka huu.