Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro amesema atatumia kurasa za mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram na Twitter na makundi ya WhatsApp ili kujua kero zao na kuzitafutia utumbuzi.
Muro amesema hayo katika mkutano wake na wa awamu ya kwanza na wananchi wa Kata ya Unyaahat, Kijiji cha Mahambe, Jimbo la Singida Mashariki.
Aidha, amesema ili kuyafikia makundi mengi atatumia pia mfumo wa kuweka taarifa kwenye ofisi za serikali za vijiji kupitia watendaji wa vijiji na kata, mikusanyiko katika madhehebu ya dini na mikutano ya hadhara itakayofanywa na viongozi wa kisiasa wabunge, madiwani na wenyeviti wa vijiji.