Kenyatta: Nimepoteza rafiki

0
239

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametoa salamu za pole kwa Serikali ya Tanzania na Watanzania wote kufutia kifo cha Rais Dkt John Magufuli kilichotokea hapo jana mkoani Dar es salaam.

Akilihutubia Taifa la Kenya kufuatia msiba wa Rais Magufuli, Rais Kenyatta amesema Kenya  imesikitishwa na kifo cha Rais Maguful.

Amesema binafsi alikuwa akishirikiana kwa karibu na Rais Magufuli na kuongeza kuwa amepoteza ndugu, rafiki na Kiongozi mwenzake.

Amesema Kenya iko pamoja na Tanzania katika kuomboleza msiba huo mkubwa na itaendelea kushirikiana na Tanzania hadi siku ya kupumzishwa kwa Dkt Magufuli katika nyumba yake ya milele.