Kenyatta akabidhi Uenyekiti wa EAC kwa Ndayishimiye

0
207

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amekabidhi Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye.

Kenyatta amekabidhi Uenyekiti kufuatia kukoma kwa kipindi chake cha uongozi katika Jumuiya hiyo.

Baada ya kukabidhiwa Uenyekiti wa EAC, Rais Ndayishimiye amesema, katika uongozi wake ataendeleza umoja uliopo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki huku akiikaribisha Somalia kuwa mwanachama mpya wa Jumuiya hiyo.

Pia amesema katika uongozi wake amesema atahakikisha amani inapatikana katika Taifa la Congo.