Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameagiza idara za elimu nchini humo kuhakikisha madarasa elfu kumi yanajengwa, ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa linalozikabili shule nchini humo.
Rais Kenyatta ametoa agizo hilo hkatika kipindi hiki ambacho shule zikikaribia kufunguliwa baada ya likizo fupi ya wiki mbili huku Walimu na Wanafunzi wakikabiliwa na shinikizo la kumaliza mitaala kwa wakati kutokana na janga la corona ambapo shule zilifungwa kwa muda mrefu ili kukwepa maambukizi.
Shule hizo zinafunguliwa huku ada na gharama nyingine zikiwa zimepanda, na Maafisa Elimu wameagizwa kuhakikisha kila shule inakuwa na hifadhi ya maji ya kutosha ili kuwezesha usafi kwa Wanafunzi vikiwemo vifaa vya kunawia maji kama hatua ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Shule hizo zinafunguliwa huku Walimu na Wanafunzi wakitakiwa kuchukua tahadhari kubwa za kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona, hasa uvaaji wa barakoa suala ambalo limewekwa kuwa la lazima.