Kenya ina mpango wa kuondoa vikosi vyake vilivyopo nchini Somalia ifikapo mwaka 2021, ili kuepuka mashambulio ya kigaidi yanayoendelea nchini humo.
Wizaya ya ulinzi ya Kenya kupitia kwa Waziri wa wizara hiyo Balozi Monica Juma, hivi karibuni itaanza mazungumzo kuona namna ya kurejesha vikosi vyake kutoka nchini Somalia, vikosi vilivyopelekwa kwa lengo la kuimarisha ulinzi nchini humo.
Vikosi vya Kenya viliingia rasmi nchini Somalia mwaka 2011 ili kuvisaidia vikosi vya nchi hiyo kukabiliana na wanamgambo wa Al Shabaab ambao wamekua wakifanya mashambulio katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na katika nchi jirani ya Kenya.
Kuendelea kwa mashambulio hayo ya Al Shabaab nchini Kenya kumechangia kupunguza idadi ya watalii wanaoitembelea nchi hiyo, kwa kuwa wengi wao wamekua wakihofia usalama wao.