Kaya 2,500 Kahama kupata maji ya Ziwa Victoria

0
138

ZAIDI ya wakazi 2,500 wa mtaa wa Mtakuja, kata ya Nyahanga katika Halmashauri ya Manspaa ya Kahama mkoani Shinyanga, wanatarajia kuondokana na adha ya ukosefu wa maji safi na salama baada ya serikali kutoa Sh. milioni 184 za kusambaza maji ya Ziwa Victoria katika mtaa huo ambao uko juu ya mlima.

Haya yamebainishwa leo na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Kahama (KUWASA), Mhandisi Allen Marwa wakati wa hafla fupi ya utiaji saini mkataba wa ujenzi mradi wa usambazaji maji na Kampuni ya Africa One Construction kwa gharama ya shilingi milioni 184, huku ukishuhudiwa na wananchi wa mtaa huo.

Amesema mradi utakamilika kwa wakati na wananchi kupata maji na kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji lakini sasa wanasogezewa huduma ndani ya kaya zao. Amemtaka mkandarasi kuzingatia masharti ya mkataba ili amalize mapema na kupewa hati zake kwa wakati.