Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Nchimbi leo Mei 29, 2024 ameanza ziara ya kikazi katika mikoa mitano ambayo ni Singida, Manyara ,Arusha, Kilimanjaro na Tanga ambapo anafuatana na Katibu wa NEC Itikadi na Mafunzo Amos makalla na Katibu wa NEC Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Rabia Hamid.
Lengo la ziara hiyo iliyoanzia Manyoni, Singida ni kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 pamoja na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.