Kapteni Mwalusako afariki dunia

0
287

Kapteni Lawrence Mwalusako, mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) amefariki dunia.
Mwalusako amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Taifa Muhimbili iliyopo jijini Dar es salaam alikokua akipatiwa matibabu.
Mipango ya mazishi ya Mwalusako inafanyika nyumbani kwake Ubungo jijini Dar es salaam.